Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, hafla tukufu ya kuadhimisha miaka sita ya kuuawa kishahidi “Makomanda wa Ushindi” na wenzao, ilifanyika siku ya Jumapili tarehe 28 December 2025, katika mji mtukufu wa Najaf Ashraf.
Hafla hii, iliyoandaliwa kwa kumbukumbu na heshima ya mashahidi Haj Qasem Soleimani, Abu Mahdi al-Muhandis na wapiganaji wenzao, na kwa kaulimbiu isemayo (Ushahidi na Utukufu), iliandaliwa kwa juhudi za kundi la wananchi wa Najaf kwa ushirikiano wa “Kamati ya Hashd al-Shaabi.”
Katika hafla hii iliyofanyika katika ukumbi wa Jumuia ya Kitamaduni ya “Qasr ath-Thaqafa,” Ayatullah Sayyid Mujtaba Husseini, mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iraq, alihudhuria na kutoa hotuba.
Hafla hii ilihudhuriwa kwa wingi na kwa hamasa kubwa na wanazuoni wa dini, wanafunzi wa elimu ya din, pamoja na makundi mbalimbali ya wananchi, na ilijumuisha programu kama hotuba, usomaji wa mashairi, na kutoa heshima kwa familia za mashahidi wa hawza.
Maoni yako